24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Raza awakingia kifua Ukawa

Na Is-haka Omar, Zanzibar
MWAKILISHI wa Uzini,

Mohamed Raza
Mwakilishi wa Uzini, Mohamed Raza (CCM)

(CCM) ameibuka na kuwakingia kifua wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kusema Serikali isipuuze madai yao.

Alisema ili kuweza kupata Katiba itakayoridhiwa na pande zote ni lazima ufikiwe muafaka wa pamoja kati ya pande mbili kama njia ya kuinusuru Katiba Mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja jana alisema endapo hoja na mawazo ya vyama vya upinzani yakipuuzwa, kuna kila dalili ya kukwama kupatikana kwa Katiba Mpya iliyokusudiwa na wananchi wa pande mbili za Muungano.

“Kwanza nataka nieleweke kuwa mimi ni muumini wa Muungano wa Serikali mbili wenye hadhi na heshima sawa kila upande, lakini nachukua fursa hii kukishauri chama changu kukaa pamoja katika meza ya mazungumzo na Ukawa ili kuweza kupata ufumbuzi wa kudumu juu ya huu mchakato wa kupata Katiba Mpya.

“Wenzetu walipotoka katika Bunge la Katiba niliwafuata na kuzungumza nao lakini walipotoa hoja zao nikabaini kuwa zimebeba mambo ya msingi kwa maslahi ya pande zote za Muungano Tanganyika na Zanzibar sasa leo iweje wanaonekana ni wasaliti,” alisema na kuhoji Raza.

Alipoulizwa kuhusu suala la wajumbe wa CCM kupeleka hoja binafsi juu ya kutaka wananchi waulizwe kama wanataka kuendelea na mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), mwanasiasa huyo alisema kwa sasa ni vigumu kuweza kuutengua kwani upo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. Kwanza kabisa Katiba mpya siyo ya wanasiasa ni ya watanzania wote(waliopo na wajao). Mjadala wowote kuhusu katiba mpya sharti uwe ndani ya mbuge la katiba mpya. Vinginevyo ni majungu.utayarishaji wa katiba mpya ulipewa utaratibu hadi kukamilika.Ukienda nje ya utaratibu huo unavuruga mambo.Kama hawataki wengine watateuliwa. Sio lazima wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles