27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Rasmi; Billnas na Nandy sasa ni mwili mmoja

*Wafunga ndoa takatifu KKKT Mbezi Beach

*Shangwe kuendelea Mlimani City

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

“Nafikiri uliumbwa kwa ajili yangu mahususi na kila nikikutazama unafanya nifikirie kuhusu harusi, nafikiri kuhusu shera, nafikiri kuhusu suti,”– sehemu ya mashairi ya Billnas kwenye wimbo wa DO ME aioshirikishwa na Nandy mwaka mmoja uliopita, ambayo leo yamekuwa kweli.

Baada ya uchumba uliodumu kwa zaidi ya miaka 10, sasa ni rasmi kwamba Mastaa wa Muziki wa Bongo Fleva, William Lyimo ‘Billnas’ na Faustine Mfinanga ‘Nandy’ hatimaye wamefunga ndoa takatifu katika kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Jumamosi ya Julai 16, 2022 wawili hao wamefungisha ndoa hiyo mbele ya mamia ya Watanzania waliofika kanisani hapo mbali ya waliokuwa wakifuatilia kwenye kituo cha TV cha Clouds na TV mtandao mbalimbali.

Wakati tukio hilo likiendelea muda wa kiapo cha ndoa ilipofika zamu ya Nandy alimwagika machozi mengi ya furaha yeye pamoja na mama yake mzazi.

Baada ya kufunga ndoa hiyo wanakwenda Kigamboni kwa ajili ya kupiga picha za kumbukumbu zitakiliyofuatiwa na sherehe katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa siku mbili zilizo pita Msanii Nandy alifanyiwa sherehe ya kuagwa katika uwanja wa Gofu wa Lugalo Dar es Salaam ambapo alitumia fursa hiyo kumtangaza Bilinas kuwa Meneja wake mpya.

Ikumbukwe kuwa wawili hao kabla ya kufikia kufunga ndoa, uchumba wao umepitia panda shuka nyingi za kimapenzi kutoka kwa watu mbalimbali hadi kusababisha baadhi ya watu kuamini kuwa wawili hao siyo wachumba tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles