THE HAGUE, UHOLANZI
MBUNGE na Kiongozi wa zamani wa kundi la waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR(), Alfred Yekatom amesafirishwa kwenda Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi binadamu.
Yekatom aliwasili mjini hapa juzi, ambapo ICC ilitoa taarifa ikisema alihusika kwenye mauaji, kuteswa watu, kuwashambulia raia na kutumia watoto kama wanajeshi.
Yekaton aliongoza kundi lililojihami kwa silaha la Wakristo baada wa waasi wa Kiislamu kuipindua serikali mwaka 2013.
Kundi hilo liliwajumuisha wanamgambo waliojulikana kama anti-Balaka.
Uhalifu dhidi ya Yekatom, ukiwemo uhalifu wa kivita unadaiwa kutendeka mwisho wa mwaka 2013 na mapema 2014.
Yekatom alichaguliwa mbunge mwaka 2016, licha ya kuwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa.
Alikamatwa mwezi uliopita wakati alipofyatua risasi akiwa bungeni na kutoroka baada ya kutofautiana na mbunge mwingine.
Hii ni mara kwanza mtu kusafirishwa kwenda ICC kutoka CAR. Chama cha kimataifa cha haki za binadamu (FIDH) kilisema hiyo ni ishara kuwa mamlaka za nchi zimejitolea kupambana na ukwepaji wa sheria.
Hatab hivyo, ghasia zinaendelea kuikumba CAR na karibu watu 40 waliuawa wakati wa ghasia siku ya Ijumaa kati kati mwa nchi hiyo.