26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ramaphosa alivyowasili nchini

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na mkewe, Dk. Tshepo Motsepe wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa saba usiku wa kuamkia leo Agosti 15. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo Agosti 15. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo,
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema. Rais Ramaphosa yuko nchini kwa ziara ya siku mbili kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini kwa Afrika
(SADC).
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akiongozana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam usiku.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles