MALE, Maldivia
RAIS wa Maldives, Abdulla Yameen, amesema kwamba amekubali kushindwa na mgombea wa chama cha upinzani, Ibrahim Mohamed Solih, katika uchaguzi wa kiti cha urais uliofanyika nchini hapa majuzi.
Akizungumza jana kiongozi huyo alisema kwamba, anayaheshimu matokeo hayo kwa kile alichodai ni kwamba wananchi wameamua kile ambacho wanakitaka.
“Wananchi wa Maldivia wameamua kile ambacho wanakitaka hivyo nayakubali matokeo ya jana. Mapema leo (jana) nimekutana na Ibrahim Mohamed Solih, ambaye wananchi wamemchagua kuwa rais wao ajaye,” alisema kiongozi huyo kupitia hotuba ambayo aliitoa kwa njia ya televisheni.
“Na ninampongeza sana kwa ushindi huo,” aliongeza rais huyo.
Hotuba ya kiongozi huyo imekuja baada ya Tume ya Uchaguzi nchini hapa kutangza juzi kwamba, Solih alipata ushindi kwa wastani wa asilimia 16.7.