– Mogadishu
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmaajo ametia saini sheria ya kuongeza muda wa kukaa madarakani kwa miaka miwili baada ya kuidhinishwa na bunge dogo la nchi hiyo.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Waziri wa Habari nchini Somalia Osmani Dubbe amesema Rais Farmajo amesaini rasmi sheria ya maalumu ya uchaguzi Jumanne jioni Bunge lilipitisha kwa kura nyingi muswada huo siku ya Jumatatu.
Muda wa kukaa madarakani kwa Rais Farmajo ulikwisha tarehe 8 mwezi Februari huku bunge likiwa limemaliza muda wake tangu mwezi Desemba.
Pia Uchaguzi wa wabunge na rais uliokuwa ukipaswa kufuata ulikumbwa na mizozo ya kisiasa.
Viongozi wa upinzani wa Somalia na majimbo ya Jubbaland na Puntlandpia baraza la seneti , walikataa uamuzi wa bunge.
Wafadhili wa Somalia, zikiwemo Marekani na Umoja wa Ulaya wamepinga uamuzi huo huku EU siku ya Jumanne ilisema uamuzi huo unaleta mgawanyo mkubwa na tishio la usalama wa nchi hiyo.