29.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Trump atetea wafuasi waliofanya fujo

 WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump ametetea wafuasi wake kwa madai ya mchango wao kwenye makabiliano yaliyotokea hivi karibuni, akisema kijana anayeshutumiwa kwa mauaji ya watu wawili huko Wisconsin wiki iliyopita na wafuasi wa Trump walioshiriki makabiliano Oregon Jumamosi, walichukua hatua hiyo kujitetea.

Trump alisema mpinzani mwenzake wa chama cha Democratic, Joe Biden hajawapinga wanaharakati wa mrengo wa kushoto wanaoshutumiwa kwa kusababisha vurugu.

Biden anaongoza kwenye kura ya maoni kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Novemba.

Jumatatu, akiwa Ikulu ya Marekani wakati anafanya mkutano na wanahabari, Trump alimlaumu Biden na washirika wake kwa vurugu zilizotokea kwenye jimbo ambalo meya na gavana ni wa chama cha Democratic.

Mwanahabari wa CNN alimuuliza rais ambaye anatoka chama cha Republican ikiwa atashutumu wafuasi wake ambao walifyatua risasi wakati wa makabiliano na waandamanaji wengine yaliyotokea mwishoni mwa juma lililopita Portland, Oregon.

Wakati wa makabiliano hayo, mtu mmoja wa mrengo wa kulia, Patriot Prayer, aliuawa na inasemekana mshukiwa amejieleza kuwa mfuasi wa kundi la antifa.

Jumatatu, polisi walimtaja mwanaume aliyepigwa risasi kuwa ni Aoron Danielson. Kufikia sasa, hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

“Naelewa kwamba kulikuwa na idadi kubwa ya watu ambao ni wafuasi, lakini hayo yalikuwa maandamano ya amani,” Trump alimjibu mwanahabari wa CNN na yeye mwenyewe amekuwa akishutumu vyombo vya habari vya Marekani kwa kupuuza maandamano yanayotekelezwa na kundi la Black Lives Matter.

Mwanahabari mwingine alimuuliza Trump ikiwa atashutumu ufyatuaji wa risasi uliotokea Kenosha, Wisconsin, ambaye inasemekana aliwahi kuhudhuria moja ya mikutano ya rais.

Kyle Rittenhouse, 17, anashutumiwa kwa mauaji ya watu watatu. Tukio hilo lililotokea wakati wa maandamano mjini humo yaliosababishwa na hatua ya Jacob Blake kupigwa risasi.

“Yote hayo tunayafuatilia, ni hali ambayo inazua maswali, mliona nilichokiona mimi, nafikiri alikuwa anajaribu kuondoka, inaonekana hivyo. Akaanguka na wakaanza kumshambulia. Na sasa hivi wanafuatilia tukio hilo, wakati uchunguzi unaendelea. Nafikiri alikuwa kwa matatizo makubwa, pengine hata angeuawa,” Trump alisema.

Mapema Jumatatu, Biden alikemea vurugu zilizotokea kwenye maandamano ya hivi karibuni huku akimlaumu rais Trump kwa kufanya nchi hiyo kutokuwa salama.

Mgombea wa Democtratic alikuwa akijaribu kujibu ukosoaji kutoka Republican kwamba anaudhaifu wa kufuata sheria na utaratibu.

“Je mimi ninafanana na msoshalisti mwenye msimamo mkali ambaye anahurumia wanaofanya vurugu?” Bwana Biden aliuliza hivyo akiwa Pittsburgh, katika jimbo muhimu kwenye uchaguzi wa Marekani la Pennsylvania. Kweli?,” alihoji.

Matamshi ya Biden yanawakilisha jinsi ambavyo amekuwa akimshambilia Trump, kwamba Ikulu ilishindwa kukabiliana na janga la virusi vya corona ambalo limesababisha vifo vya watu zaidi ya 180,000 nchini Marekani.

Kulingana na gazeti la Washington Post kuthibitisha ukweli, awali,Biden alipinga maandamano ya vurugu mara kadhaa kati ya Mei na Julai.

Lakini wakati wa mkutano wao, chama hicho hakikizungumzia suala hilo badala yake kilijikita zaidi kwenye ubaguzi wa rangi na madhila wanayopitia Wamarekani weusi mikononi mwa polisi. Aidha,wiki moja baadae, ghasia na uporaji ndio maudhui yaliyotawala mkutano wa Republican.

Tukio la kupigwa risasi kwa Blake huko Wisconsin Agosti 23, limesbabisha maandamano huku Bwana Biden na timu yake ya kampeni wakianzisha tena ukosoaji dhidi ya maandamano yenye vurugu.

 Hata hivyo utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha sheria cha Marquette, Milwaukee, Wisconsin, Agosti 11, ulibaini kwamba wanaounga mkono maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi wamepungua kwa asilimia 13 huku umaarufu wa kundi la Black Lives Matter ukipungua kwa asilimia 10, kuanzia Juni hadi Agosti.

Wisconsin, eneo muhimu kwa Trump lakini pia ni jimbo ambalo ushindi wake katika uchaguzi wa Novemba, kwa hakika unakwenda kwa chama cha Democratic.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles