27.5 C
Dar es Salaam
Friday, July 1, 2022

Lissu aeleza mikakati yake

GRACE MACHA -ARUSHA 

MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ameahidi kulifanya Jiji la Arusha kuwa la viwanda kwa ukanda wa mikoa ya Kaskazini, endapo atachaguliwa kuwa rais. 

Alisema kuwa Arusha ilikuwa na viwanda vya matairi, nguo na vingine vingi, lakini vimekufa. 

Aidha ameahidi akiingia madarakani atahakikisha inapatikana Katiba mpya ya wananchi itakayompunguzia rais madaraka. 

Lissu pia ameahidi kufumua sera na mfumo wa kodi unaotumiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuweka utakaowezesha biashara kustawi na kukuza uchumi wa nchi. 

Aliyasema hayo juzi, wakati akiongea na wananchi waliojitokeza kumsikiliza kwenye viwanja vya Relini jijini Arusha, akiwa ameambata na mgombea mwenza, Salum Mwalimu pamoja na viongozi wakuu wa chama hicho. 

Lissu alisema atarejesha Jiji la Arusha kuwa la kidiplomasia. 

Alisema kuwa wakati akiwa na umri wa miaka 15 hadi 30 alikuwa akiishi Arusha na ilikuwa ikitambulika kama Geneva ya Afrika. 

“Viongozi wa Afrika walipotaka kukutana walikuja kwenye jiji hilo na viongozi wa dunia walipotaka kujadili masuala ya Afrika walikuja, lakini mambo yamebadilika, hakuna mikutano hiyo,” alisema Lissu. 

Lissu alisema Arusha ulikuwa ni mji mkuu wa utalii Afrika, ambao pamoja na miji jirani ulikuwa kitovu cha utalii na taifa lilinufaika sana na mapato yatokanayo na utalii. 

“Serikali yangu itatengeneza mahusiano na dunia ili watalii waje kwa 

 wingi,” alisema Lissu. 

Alisema akichaguliwa atafanya marekebisho makubwa ya sheria kwenye makosa ya kijinai, ikiwemo ile inayonyima dhamana kwa watuhumiwa wa baadhi ya makosa, ikiwemo yale ya utakatishaji fedha haramu, uhujumu uchumi na ugaidi. 

Lissu alisema watoto wanafundishwa kufaulu mitihani na hata wazazi wanawatafutia shule zinazofaulisha badala ya kuwajengea uwezo kupata maarifa ya kuwawezesha kuyatumia kwenye maisha yao. 

“Ili taifa liendelee, nikiingia madarakani itabidi kubadili mfumo wa elimu tuwafundishe watoto wetu stadi za kazi ziweze kuwasaidia kwenye maisha. 

“Nimetembea nchi mbalimbali, si lazima mtu afaulu mtihani kuwa ndiye mwenye akili, kuna watu wana maarifa,” alisema Lissu. 

Alisema kuwa akiingia madarakani atahakikisha wananchi wote wanakuwa na bima ya afya ambayo itapatikana kwa bei ndogo, itakayowawezesha kupatiwa matibabu ya magonjwa yote. 

“Tatizo la afya ni kubwa nchi hii. Mimi baada ya kukaa miaka mitatu nikipatiwa matibabu kwenye hospitali mbalimbali, nikiingia madarakani nitahakikisha kila mtu ana bima. 

“Nilipoumizwa nikavunjwavunjwa kila mahali, nilipofika Ubelgiji hawakuniuliza fedha, waliniuliza bima ya afya iko wapi nikawaambia sina, wakaniambia ni lazima uwe na bima ya afya. 

“Kule bima zinatolewa na vyama vya siasa. Nikaenda kwenye Chama cha Christian Democrats nikalipa fedha zisizofika Sh milioni 1 kwa ajili yangu na mke wangu na nikapata matibabu bora kabisa. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,419FollowersFollow
544,000SubscribersSubscribe

Latest Articles