31 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia awatoa hofu wananchi kuhusu kupanda kwa mafuta

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali iko macho katika kuangalia bei ya mafuta nakwamba inajitahidi kuhakikisha kuwa haipandi kama ilivyo kwenye nchi nyingine.

Kauli ya Rais Samia imekuja kufuatia kupewa vilio vya bei ya mafuta na wananchi wa Mbalizi mkoani Mbeya katika ziara yake ya siku nne mkoani humo iliyoanza leo Agosti 5, 2022.

Ikumbukwe kuwa mwanzoni mwa wiki hii Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), ilitangaza bei mpya za ukomo wa mafuta, ikionesha Jiji la Dar es Salaam lita moja ya petroli ni Sh 3,410 huku dizeli ikiunzwa kwa Sh 3,322 na mafuta ya taa Sh 3,765.

Rais Samia amesema mafuta ya kula na petroli yalikuwa yameadimika, lakini Serikali tayari imepatia ufumbuzi hatua ambayo imeleta unafuu wa bei.

Aidha, Rais Samia amekiri kuwa mafuta ya gari bado ni changamoto kubwa kutokana na kupanda zaidi kwenye soko la dunia hatua inayochochewa na vita ya Urusi na Ukraine.

“Serikali inatoa Sh bilioni 100 kila mwezi, ili bei zibaki hivyo zilivyo, tukiacha bei ya dunia itakuwa ghali sana, mafuta ni duniani kote mpaka waache kupigana, ndio tutarudi kuwa sawa,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ameongeza kuwa: “Ndugu zangu kwenye mafuta serikali tupo macho, tunajitaidi kufanya bei isipande zaidi kama wenzetu. Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki kuna nchi mafuta hayanunuliki.

“Niwakumbushe kuwa tatizo la mafuta ni la dunia nzima, serikali bado tunaendelea kuangalia, isingekuwa hivyo shilingi bilioni 100 zingeingizwa kwenye miradi ya maendeleo,” amesema Rais Samia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles