24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia awataka viongozi mkoani Kagera kusimamia vizuri fedha za maendeleo

*Bashe aahidi neema kwa wakulima

Na Renatha Kipaka, Biharamulo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi kusimamia vizuri matumizi ya fedha ili yanufaishe Wananchi.

Rai Samia ametoa agizo hilo Juni 8, 2022 wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Biharamulo baada ya kuanza ziara yake ya kikazi ya siku tatau mkoani Kagera.

Amesema ataendelea kufanya ushirikiano na viongozi katika jitihada za kuleta mafanikio kwa Wananchi wake ili kutimiza ndoto zao.

“Niwaombe viongozi mkasimamie vizuri matumizi ya fedha ili yanufaishe wananchi wetu, nami nitaendelea kufanya ushirikiano na viongozi ili kuhakikisha kuwa malengo tuliyojiwekea yanakamilika,” amesema Rais Samia.

Awali akitoa salamu kwa wananchi Waziri wa Maji, Jumaa Awesu amesema katika upande wa kusaidia akina mama kutotembea umbali mrefu kutafuta maji, Serikali imeleta miradi 78 na tayari 38 imetekelezwa.

Amesema, sasa nchi mzima ipo miradi 1,176 itatekelezwa na kusaidia wananchi wanaopata shida ya huduma ya maji.

Wakati huo huo Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe amesema katika zao la pamba tayari serikali imeondoa makato ya pembejeo na mbegu.

“Ndugu zangu wakulima msikubali kukatwa makato ya pembejeo na mbegu kwenye zao la pamba kwani serikali imeondoa na kupanga mauozo ya Sh 1,560 hadi 1,900 kwa kilo.

“Wakulima wa Biharamulo mnaolima zao la pamba mtauza zao hilo wilayani Chato mkoani Geita kwani kuna jineli,” amasema Bashe.

Ameongeza kuwa zao la kahawa kupitia mnada uliofanyika June 7, mwaka huu wilayani Ngara mkoani Kagera mkulima aliuza kwa Sh 3,720.

“Nitumie nafasi hii kuwaambia kuwa Kilimo sio umaskini bali ni biashara na tayari wananchi wa mkoa wa Kagera waliambiwa kutenga hekta 6,200 kwa kilimo cha mchikichi hii ni katika kuboresha shuguli ya kilimo na kunufaisha mkulima,” amesema Bashe.

Bashe ameongeza kuwa maeneo ya minada mkulima atauza kwa gharama ya ushindani wa Sh 1,650 kwani muda wa kuwaibia Wananchi umeisha

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles