23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia afanikisha muafaka Kariakoo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

UAMUZI wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kuwatuma wasaidizi wake wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa umetoa nafasi kwa wafanyabiashara wa soko la Kariakoo jijni Dar es Salaam kueleza dukuduku lao na mwisho kutoka na muafaka kwa kukubaliana kuendelea na biashara.

Itakumbukwa mapema jana Mei 17, 2023 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na timu yake ya mawaziri wa sekta husika, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Dk. Ashatu Kijaji na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alfayo Kidata alitimiza ahadi yake ya kukutana na wafanyabiashara hao viwanja vya Manazi Mmoja, kama alivyowaahidi Mei 15, mwaka huu.

Mara baada ya kikao chao cha jana chini ya Waziri Mkuu wafanyabiashara hai waliafiki kusitisha mgomo baada ya Serikali kutanganza kuunda Tume ya watu 14 kutoka Serikalini na wawakilishi wa wafanyabiashara kwa ajili ya kufanyia kazi yale yaliyowasilishwa na kupendekezwa na wafanyabiashara hao.

Aidha, Serikali imetoa maelekezo tisa ikiwemo kusitisha kabisa shughuli zilizokuwa zikifanywa na Task Force (kikosi kazi) kilichokuwa kimeundwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kufanikisha ukusanyaji mapato.

Akizungumza na wafanyabiashara hao baada ya kusikiliza dukuduku zao, Majaliwa alisema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuthamini sekta ya biashara amefungua milango ya kufanyika biashara na malengo hayo yameanza kufanikiwa.

Alisema hoja zote zilizotolewa kwenye kikao cha jana wanaendelea kuzifanyia kazi, lakini zitafanyiwa kazi kwa mfumo shirikishi na kazi hiyo siyo ya Serikali peke yake.

Alisema ili kufanikisha hillo ni lazima kuwe na Tume ya pamoja na kukumbushana yale waliokubaliana na yale yatakayosaulika ili yaweze kufanyiwa kazi.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles