28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Philippines awataka raia wawauwe wahalifu

Mayor Rodrigo DuterteMANILA, PHILIPPINES

RAIS mteule wa Philippines, Rodrigo Duterte ameuhimiza umma kumsaidia katika vita yake dhidi ya uhalifu na kuwataka raia wanaomiliki silaha kuwapiga risasi na kuwaua wauzaji wa dawa za kulevya.

Ametoa idhini hiyo kwa raia kujichukulia sheria mkononi dhidi ya wahalifu wanaopinga kukamatwa au wanaozusha mapambano katika maeneo yao.

“Mjihisi huru kutupigia simu au maafisa wa polisi; au kwa mnaomiliki bunduki wafyatulieni risasi na nitawapa zawadi kwa kufanya hivyo,” Duterte aliwaambia wafuasi wake katika hotuba ya kusherehekea ushindi iliyotangazwa moja kwa moja kwenye televisheni katika mji wa kusini wa Davao.

Duterte pia amewataka majenerali watatu wa polisi walioko katika kambi ya taifa ya polisi mjini hapa  kujiuzulu mara moja kutokana na ushiriki wao katika uhalifu ambao hakuutaja. Alitishia kuwaumbua hadharani iwapo hawatajiuzulu wenyewe.

Duterte mwenye umri wa miaka 71, alishinda uchaguzi wa rais uliofanyika Mei 9, 2016 kwa ahadi ya kukomesha uhalifu na rushwa ndani ya kipindi cha miezi sita. Anatarajia kuapishwa kuanza kazi rasmi Juni 30, 2016.

Lakini makundi ya haki za binaadamu yameelezea hofu kwamba kampeni yake ya kukomesha uhalifu huenda ikasababisha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Duterte anatarajia kuapishwa kuanza kazi rasmi Juni 30, 2016.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles