Na RASI INNO NGANYANGWA
KAMA kuna wengi wanaofahamu kuhusu ‘Back’ yake katika kuzimikia muziki nina hakika ni wachache sana kutokana na hulka yake ya ‘non nosense’ tangu kitambo akiwa katika nafasi mbalimbali za uwaziri.
Lakini hiyo sio ishu ninayotaka tuisanukie hapa leo kwani politiki siyo mahala pake katika safu hii, ila akiwa kama mkuu wa taifa kuna hisia zilimgubika akaweka wazi kwamba hazimikii masuala ya masholi kujiachia kihasara kwenye vichupa.
Kwa hali ilivyo ni kwamba huwezi kucheki kichupa na mtu unayempa respect kubwa manake jinsi video vixens wanavyojiachia inaleta hisia nyingine zisizotakiwa hadharani ambazo mahala pake ni faraghani.
Wakati akipiga nondo hiyo alikuwa akinena na wanachama wa CCM kwenye mkusanyiko wao kule Dodoma, tangu hapo alichokianzisha kikashika kasi hata walio chini yake wakawa wanapigia upatu.
Prezidaa alinena kwamba hata yeye anazimikia sana mangoma ila vichupa vinamboa kutokana na mambo hadharani yanayofanyika ambayo hayafai!
Ikanipa aidia kwamba nikague vichupa kadhaa vinavyoruka hewani kwenye runinga ambavyo katika ‘Back’ hiyo ilikuwa poa tu katika awamu zilizopita, kwamba ilikuwa kawaida tu kuwa kihivyo lakini tangu mkubwa aseme yake kuhusu hiyo ishu kuna vichupa kadhaa katika ‘Front’ iliyofuata vimejikataa vyenyewe.
Hata kama vikilazimishwa kuwekwa kwenye kioo cha runinga ama vitakatizwa chata la utata linapokaribia au vitafanyiwa mixing ya kiaina ili kuziba au kichupa kingine kinapandishwa juu yake na kukiziba kichupa fyongo.
Hiyo maana yake ni kwamba kuna wasanii kadhaa itabidi watengeneze video mpya kwani zilizowapaisha kama zina mambo ya misanuko aliyokemea Prezidaa mida ya sasa katika ‘Front’ hii sio mwake kabisa!
Hapo mambo ya bajeti yanahusika na kama nd’o ilikuwa ya unga unga mwana basi lazima kwenye ‘Front’ mpya kuna wasanii watabonyea kwa muda.
Hii ishu imenirudisha ‘Back’ nyakati flani ilipoaminika kwamba ‘obscenity sales’ kwamba misanuko wazi inauza! Lakini kama kila kitu ni kukopi na ‘ku-paste’ basi kiaina tunatokota, maana sio kila kitu cha kukopi, kwani hata huko mbele kuna maneno yanayotumika kwenye mistari tangu kitambo hadi sasa utayakuta kwenye mauzo ya kitaani.
Sio kwenye kucheki kwa ujumla kama ambavyo neno ‘F’ lisivyotumika kila mahala kama inavyodhaniwa ndiyo maana kule wana ‘system’ ya kudhibiti kisichotakiwa kuchekiwa na madogo ili wasipagawe tangu mapema.
Prezidaa sio myuzishen ila anazimikia tu mangoma lakini amegusa na katika ‘Front’ hii lazima jambo lifanyike manake kuna wasanii ni kama wanasukuma muziki wao kwa kujianika, kana kwamba hiyo ndiyo biashara halisi kumbe ni kinogesho tu uhalisia uko kwenye mikong’osio yenyewe.
Kwenye kadanse ndiko ‘live’ misanuko hatari ya madensa wa kike hujitokeza lakini kwenye kizazi kipya huanzia kwenye vichupa, hata kama uko homu na madogo inakulazimu kubadili chaneli kukwepa msala wasikuulize kisha ukashindwa kuwajibu.
Madogo wa leo sio kama wa zamani zile kwani kama wasanii wanajiita kioo cha jamii basi kimewapasukia usoni!