23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 5, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Kim Jong asafiri kwa treni kukutana na Trump

PYONGYANG, Korea Kaskazini

KIONGOZI wa nchi hii, Kim Jong-un, juzi aliondoka kwa kutumia usafiri wa treni kwenda katika mji wa Hanoi kwa ajili ya mazungumzo na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Mkutano kati ya Marekani na Korea Kaskazini unatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano na Alhamisi katika mji huo mkuu wa Vietnam.

Mkutano huu unakuja baada ya wa kwanza wa kihistoria uliofanyika mwaka jana nchini Singapore na macho yote yatakuwa yakitazama kama kuna hatua yoyote iliyopigwa tangu wakati huo kuhusu kuteketeza silaha za nyuklia.

Taarifa zilizopatikana mji  hapa zinaeleza kuwa Rais Kim Jong-un amesafiri na dada yake, Kim Yo Jong na mmoja kati ya washauri wake muhimu, Jenerali wa zamani, Kim Yong Chol.

”Tulipendana,” Trump aliuambia mkutano Septemba mwaka jana kuhusu Kim.” Aliniandikia barua nzuri,” aliongeza kiongozi huyo.

Hata hivyo, pamoja na maneno hayo mazuri, miezi kadhaa baada ya mkutano wa Juni mwaka jana, ilitawaliwa na kauli za msuguano na mahusiano yasiyoridhisha.

 Mkutano huu unatarajiwa kuendeleza misingi ya mkutano uliopita kuhusu masuala ya silaha za nyuklia, ambapo wataalamu wanasema jitihada zilizofanyika ni kidogo na kwamba zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mkutano huo wa Hanoi, ajenda zake hazijawekwa wazi.

Wachungizi wa masuala ya kisiasa wanasema kwamba, licha ya mkutano wa Juni mwaka jana nchini Singapore kati ya viongozi hao kuwa ulikuwa ni wa kihistoria, lakini makubaliano waliyoyatia saini hayakuwa dhahiri na hatua kidogo zimechukuliwa kuhusu lengo la kukomesha silaha za nyuklia.

Wanasema katika mkutano huo, Rais Trump aliahidi kukomesha vitendo vya majaribio ya silaha za nyuklia, akishirikiana na Korea Kusini ambavyo vimeighadhabisha Korea Kaskazini, lakini miezi imepita sasa wengi wakihoji yeye amefanya nini kwa upande wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles