30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Sendeka nchi imepiga hatua kusimamia gesi

Elizabeth Kilindi,Njombe.

MKUU wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amesema nchi imefanya mapinduzi makubwa ya kudhibiti na kusimamia sekta ya gesi asilia, baada ya mwisho wa mwaka 2015 kufanikiwa  kupata gesi kiwango cha futi za ujazo tilioni 55.

Aliyasema hayo wakati akifungua semina elekezi juu ya wajibu wa Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ambapo alisema kiwango hicho, kimeifanya Serikali kujenga bomba la kusafirishia mafuta  kutoa Mtwara  hadi Dar es Salaam.

‘’Hiki ni kiwango cha juu, kazi iliyobaki ni kuendelea kuhakikisha gesi inatumika katika nyumba mbalimbali miji mengine ya karibu ambayo inaweza kufikiwa na gesi hiyo’’alisema Ole Sendeka.Alisema jukumu kubwa la mamlaka hiyo, ni kuendelea kusimamia sekta ndogo zote ili kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa udhibiti na usimamizi.

‘’Kutoakana na kukua kwa shughuli za kiuchumi utakubaliana nami kwamba utaratibuu wote wa misingi ya utawala bora unaweka mgawanyo wa majukumu haya kati ya serikali,mdhibiti mwenyewe na watoa huduma,kwa hiyo sasa serikali itaendelea na jukumu lake la uwekaji wa sera na mdhibiti ambaye ni Ewura ataendelea na shughuli zake za udhibiti na usimamizi na watoahuduma wataendelea kutoa huduma  wakisimamiwa kwa mujibu wa sheriana kanuni zilizowekwa’’alisema Ole Sendeka.

Alisema suala la kusimamia udhibiti na usimamizi, linahitaji watumishi wa umma ambao kwa matendo yao wanahakisi taswira halisi ya serikali ya awamu ya tano kwa kuonyesha uwaminifu wao,uadilifu wao na utiifu kwa kiwango ambacho anaepewa huduma au anaesimamiwa.

‘’Si ofisa awe ametoka Dar es Salaama au ya ofisi ya kanda njanda za juu kusini, bali  kwa yoyote wa serikali aliyepewa dhamana kuendelea kusimamia kufanya udhibiti wa utoaji wa huduma hizi ambazo tumezitaja…swala la uzalendo, linajumuisha upendo wa dhati wa mtu na kwa watu wake ambao watumishi wa umma uzalendo ni pamoja na kuenda matendo mema kwa wale unaowahudumia wanaridhika na kuondoka bila ya manung’uniko,’’alisema Ole Sendeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles