26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 3, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS KENYATTA AHUTUBIA BUNGE, WAPINZANI WASUSA

NAIROBI, KENYA


RAIS Uhuru Kenyatta, amehutubia kikao cha kwanza cha Bunge la 12 la Kenya mjini hapa jana.

Katika kikao hicho kilichosusiwa na wabunge wa upinzani unaodai kutomtambua, Rais Kenyatta aliwahakikishia Wakenya na jumuiya ya kimataifa kwamba Kenya hakuna ombwe la uongozi.

Alisema katiba iko wazi, kwamba kipindi cha rais kinaisha wakati mwingine anapoapishwa.

“Muhula wa urais unakoma hadi mwingine anapoapishwa kwa mujibu wa katiba. Nataka kuwahakikishia Wakenya na dunia kwamba kila mhimili wa Serikali uko mahala pake na shughuli zinaendelea kama kawaida. Hakuna ombwe,” alisisitiza.

Alisema wabunge wameapishwa katika kipindi ambacho kinawataka waheshimu demokrasia.

Alirudia msimamo wake kuwa anatofautiana vikali na uamuzi wa Mahakama ya Juu kufuta matokeo yaliyompa ushindi, lakini aliuheshimu kwa vile anaheshimu katiba na taasisi zake.

“Nimeonyesha hili kabla, wakati nilipokubali kushindwa mwaka 2002 na kuitikia mwito wa mahakama ya kimataifa wakati nikijua nakabiliwa na mashtaka porojo,” alisema.

Aliwataka wabunge kuhakikisha uendelevu wa demokrasia kwa kuendeleza amani.

Alionya kwamba hakuna mtu atakayeruhusiwa avuruge amani na kuwataka viongozi wa kisiasa kukwepa kutoa matamshi ya kichochezi.

Mbali ya wabunge wa upinzani waliosusa, majaji wa Mahakama ya Juu pia walikosekana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles