28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Rais aifuatilia Nigeria akiwa Ikulu

ABUJA, NIGERIA

MITANDAO ya kijamii ya michezo nchini Nigeria juzi, ilikuwa inamuonesha rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari akiwa Ikulu anaufuatilia mchezo dhidi ya Burundi.

Michuano hiyo imeanza kutumua vumbi tangu Ijumaa wiki iliopita, huku timu ya Nigeria ikitupa karata yake ya kwanza katika hatua ya makundi juzi na kushinda bao 1-0, lililofungwa dakika ya 77 kutoka kwa nyota wao Odion Ighalo.

Msaidizi wa rais aliposti picha hiyo ikimuonesha akiwa makini akifuatilia mchezo huo kwa kupitia runinga, hivyo mashabiki walionekana kufurahia kuona kiongozi huo akiwaangalia vijana wake.

“Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, akiufuatilia mchezo wa kwanza wa timu hiyo kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Burundi,” waliandika chini ya picha hiyo.

Katika mchezo mwingine unaofuata, Nigeria inatarajia kushuka dimbani dhidi ya Guinea ambapo nahodha wa timu hiyo Obi Mikel amedai watahakikisha wanashinda ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua inayofuata.

“Tumeshinda dhidi ya Burundi lakini haikuwa kazi rahisi, tutahakikisha tunaendelea kushinda michezo iliobaki ili kujihakikishia nafasi ya kuingia hatua inayofuata,” alisema mchezaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles