Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika amejiuzulu wadhifa wake baada ya miaka 20 kufuatia wiki kadhaa za maandamano nchini mwake.
Bouteflika amekuwa madarakani kama rais kwa muda wa miaka 20, tayari alikuwa amefutilia mbali mpango wa kugombea muhula mwingine kutawala kutokana na kukuwa kwa upinzani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la nchi hiyo, kiongozi huyo tayari aliondoa mipango yake ya kusaka awamu ya tano madarakani, wakati upinzani dhidi ya Serikali yake ukiongezeka.
Jeshi la Algeria ambalo lina nguvu, lilimtaka kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kutangaza kuwa hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya uongozi.
Abdelaziz Bouteflika alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi, miaka sita iliyopita na tangu hapo mara chache amekuwa akionekana katika sehemu za umma.
Rais Abdelaziz Bouteflika,aliweza kutoa taarifa hizo rasmi kwa mujibu wa katiba inayoruhusu rais kusitisha muda wake wa kutawala”
Uamuzi huo wa Rais Bouteflika ulitangazwa pia na Televisheni ya Taifa ya nchi hiyo.