31.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Raila kuunda muungano wa vyama vitano

Raila-Amolo-OdingaNAIROBI, KENYA

KINARA wa chama cha upinzani cha ODM, Raila Odinga, anafanya mazungumzo na viongozi wa vyama vitano vya kisiasa ili kuunda muungano mkubwa na thabiti utakaoweza kumng’oa madarakani Rais Uhuru Kenyatta katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Maelezo kuhusu mazungumzo hayo ya siri yameanza kuibuka huku washirika wa karibu wa Odinga wakizungumzia kuhusu wanachotaja kuwa ‘mama wa miungano yote’.

Washirika hao wameeleza matumaini makubwa kuwa muungano wanaopanga kuunda utakuwa na nguvu za kutosha kumshinda Rais, Uhuru Kenyatta.

Walisema wengine ni Kiongozi wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, Kiongozi wa Chama cha Amani National Congress (ANC), Musalia Mudavadi na mwenzao wa Kanu, Gideon Moi ni nguzo muhimu katika muungano huo.

Wametaja vyama vingine wanavyolenga kuwa ni NARC, kinachoongozwa na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Charity Ngilu na NARC Kenya cha Martha Karua.

Mmoja wa viongozi wa upinzani, alisema Odinga na washirika wake wakuu katika muungano wa Cord wameshauriwa waachane na muungano huo ulioundwa mwaka wa 2012.

Inasemekana Odinga ametambua kuwa jaribio lake la tatu la kuwania urais mwaka 2013 lililemazwa zaidi na kuondoka kwa washirika wenzake kwenye kundi lililokuwa likijulikana kama Pentagon.

Kundi hilo lilimhusisha Naibu Rais, William Ruto na liliparanganyika baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa iliyotokana na ghasia za baada ya Uchaguzi Mkuu wa maka 2007.

Wabunge Junet Mohammed (Suna Mashariki) na Ayub Savula (Lugari) walithibitisha kuwa kuna mazungumzo ya kuunda muungano mpya na kwamba Odinga amekuwa akizungumza na viongozi hao.

“Naweza kukuthibitishia kuwa Odinga, Mudavadi, Moi na Musyoka wako kwenye mazungumzo muhimu ya kuunda muungano mkubwa wa kuwaondoa Wakenya katika lindi la ufisadi,” alisema.

Mazungumzo hayo yakishindikana basi hakuna atakayefanikiwa katika uchaguzi huo,” alisema Mohammed.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles