MOSCOW,Urusi
RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amesema yupo tayari kukutana na mwenzake wa Marekani Donald Trump kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kidiplomasia.
Taarifa iliyotoliwa jana mjini hapa, kiongozi huyo alitoa taarifa hiyo kupitia barua aliyomwandikia Trump na akamweleza kuwa uhusiano baina ya mataifa haya mawili ni muhimu sana.
“Katika barua hiyo Rais Putin alisisitiza kuwa uhusiano wa Urusi na Marekani ni jambo muhimu zaidi kwa kuandaa utulivu wa kimkakati na usalama wa kimataifa,” alieleza taarifa hiyo ya Kremlin iliyotolewa jana
“Alithibitisha kuwa Urusi ipo wazi kwa majadiliano na Marekani katika ajenda pana zaidi,”iliongeza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ya Putin imekuja baada ya mwishoni mwa Novemba Rais Trump kufuta mkutano wao ulipangwa kufanyika nje ya mkutano wa nchi tajiri 20 duniani (G20) uliofanyika nchini Argentina,akielezea kusononeshwakwake na majeshi ya Urusi kuzishambulia meli ya kikosi cha wanamaji cha Ukraini na kisha kuziteka.
Mwisho