27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Putin akubali kukutana na Trump

MOSCOW,Urusi

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amesema yupo tayari kukutana na mwenzake wa Marekani  Donald Trump kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kidiplomasia.

Taarifa iliyotoliwa jana mjini hapa, kiongozi huyo alitoa taarifa hiyo kupitia barua aliyomwandikia Trump na akamweleza kuwa uhusiano baina ya mataifa haya mawili ni muhimu sana.

“Katika barua hiyo Rais  Putin alisisitiza kuwa uhusiano wa Urusi na Marekani  ni jambo muhimu zaidi kwa kuandaa utulivu wa kimkakati na usalama wa kimataifa,” alieleza taarifa hiyo ya  Kremlin iliyotolewa jana

“Alithibitisha kuwa Urusi ipo wazi kwa  majadiliano na Marekani katika ajenda pana zaidi,”iliongeza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ya Putin imekuja baada ya mwishoni mwa Novemba Rais Trump kufuta mkutano wao ulipangwa kufanyika nje ya mkutano wa nchi tajiri 20  duniani (G20) uliofanyika nchini Argentina,akielezea kusononeshwakwake na majeshi ya Urusi kuzishambulia meli ya kikosi cha wanamaji cha Ukraini na kisha kuziteka.

Mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles