25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

PSG WAKO TAYARI KUMPELEKA NEYMAR MADRID

PARIS, UFARANSA

HATIMAYE Rais wa klabu ya PSG, Nasser Al-Khelaifi, amefunguka na kuweka wazi kuwa wapo tayari kumwashia taa ya kijani mshambuliaji wao, Neymar ya kujiunga na Real Madrid mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.

Hata hivyo, rais huyo amedai kwamba, mipango hiyo inaweza kukamilika endapo mchezaji huyo atapambana na kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

PSG wamedai kuwa hawatakuwa na kinyongo kwa mchezaji huyo kuondoka kama tayari watakuwa wametwaa taji hilo, lakini kama itashindikana msimu huu kuchukua taji hilo, basi inaweza kuwa ndoto kwa mchezaji huyo kuondoka mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.

Neymar alijiunga na klabu ya PSG kwa kitita cha pauni milioni 198 mkataba wa miaka mitano, akitokea klabu ya Barcelona wakati wa majira ya joto mwaka jana, lakini kwa sasa tayari ameanza kuonesha dalili za kutaka kurudi nchini Hispania.

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, wameonesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo tangu kipindi hiki cha uhamisho wa Januari, lakini dili hilo linaweza kuwa gumu kwa siku zilizobakia.

Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajia kuendelea mwezi ujao, huku PSG wakiwa na kibarua kizito cha kuhakikisha wanawatoa mabingwa watetezi Real Madrid kwenye hatua ya 16 bora.

“Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunatwaa taji la Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu nchini Ufaransa, Neymar anaweza kuondoka wakati wa majira ya joto kama tutafanikiwa kutwaa taji hilo, lakini atabaki endapo tutashindwa kutwaa,” alisema Al-Khelaifi.

Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez, kwa upande wake ameweka wazi kuwa anaweza kuachana na mshambuliaji wake hatari, Cristiano Ronaldo, ili kuipata saini ya Neymar wakati wa kiangazi.

Real Madrid wamesema wapo tayari kuvunja rekodi ya usajili ambayo imefanywa na PSG kwa kumsajili Neymar, huku wao wakisema wanaweza kuweka mezani kitita cha pauni milioni 218 ili kumsajili mchezaji huyo.

Msimu huu Madrid wamekuwa kwenye kiwango cha chini huku wakiwa nyuma kwa pointi 19 dhidi ya wapinzani wao Barcelona ambao ndio vinara wa Ligi Kuu nchini Hispania, ila Madrid ambao ni mabingwa watetezi wanashika nafasi ya nne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles