24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Program ya AFDP kuchochea maendeleo Sekta ya Kilimo, Uvuvi

Na Mwandidhi Wetu, Mtanzania Digital

KATIBU MKUU Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dk. Jim Yonazi amesema Serikali imedhamiria kuendelea kuwekeza katika sekta ya kilimo na uvuvi kwa lengo la kuchagiza maendeleo kupitia miradi inayotekelezwa na program ya kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi ya AFDP nchini.

Ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Morogoro Mjini na Kilosa Mkoani Morogoro alipotembelea na kukagua shughuli za utekelezaji wa program hiyo inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Katika ziara yake ametembelea Taasisi za Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA),Taasisi ya utafiti wa Mbegu (TARI), Taasisi ya udhibiti Ubora wa Mbegu (Tosci) pamoja na kukagua kituo Cha Viumbe Maji(DAQ) Kingolwira ikiwa ni sehemu ya maeneo yanayotekelezwa na program hiyo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jim Yonazi akiangalia moja na mapipa ya kuhifadhia maji katika maabara ya kutotoresha vifaranga vya samaki katika Kituo cha Viumbe Maji (DAQ) kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa program ya kilimo na uvuvi ya AFDP inayoratibiwa na ofisi yake.

Dk. Yonazi amesema uwekezaji huo utachangia kuongeza uzalishaji katika kilimo na uvuvi hivyo  kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na kuifanya kuwa na chakula cha kutosha

Aliongezea kuwa uwekezaji huo utawasaidia wananchi kuendelea kujifunza katika maeneo yanayotekeleza miradi hii kujiletea maendeleo yao.

“Maeneo yanayotekelezwa miradi ya AFDP yataleta chachu kwa wananchi kujifunza na kujipatia maarifa yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi hivyo itumieni miradi hii kama fursa ya kipekee,”alisema Dk. Yonazi.

Mtendaji Mkuu Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dk. Sophia Kashenge akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jim Yonazi mimea ya michikichi katika shamba la mbegu Msimba Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa program wa kuendeleza kilimo na uvuvi ya AFDP inayoratibiwa na ofisi yake.

Naye Mtendaji Mkuu Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dk. Sophia Kashenge alieleza kuwa, Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kuongeza tija katika kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi kupitia miradi mbalimbali hivyo wataendela kuunga mkono jitihada hizo kwa vitendo huku akibaini mafanikio yaliyofikiwa na taasisi yake.

“Tumejipanga kuhakikisha kunaendelea kuwekeza katika sekta yakilimo mafanikio yatokanayo na sekta hii, ASA itaendelea kuwa na mbegu bora zenye kukidhi mahitaji yaliyopo,”alisema Dk. Sophia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles