28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mkumbo: Dk. Slaa, wenzake wamekamatwa kwa makosa ya uchochezi

*Asema taratibu zote za kisheria zimefuatwa

Na Mwandishi Wetu,Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amebainisha kuwa, suala la mkataba wa uendelezaji wa bandari ya Dar es Salaam siyo sababu ya kukamatwa kwa, Wakili Boniface Mwabukusi, Balozi Dk. Wilbrod Slaa na Mdude Nyagali bali watatu hao wamekamatwa kutokana na tuhuma mbalimbali za makosa ya kijinai kama ambavyo imeelezwa na jeshi la polisi nchini.

Dk. Willbrod Slaa.

Prof. Mkumbo ameeleza hayo alipohojiwa na Idhaa ya Kingereza ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na kuongeza kuwa, kama kukosoa uwekezaji wa bandari ndio sababu ya kukamatwa basi watu wengi wangekuwa wamekamatwa hadi sasa.

Amesema Tanzania ni nchi inayofuata utawala wa sheria hivyo amezitaka jumuiya za kimataifa kuiheshimu Tanzania na utawala wa sheria uliopo nchini na wanapaswa kutoa madai yao pale tu sheria zilizopo hazifuatwi na si vinginevyo.

“Tanzania ni nchi yenye kufuata utawala wa sheria ni nchi ambayo inafuata sheria zake. Jumuiya za kimataifa zinazohusiana na haki za binadamu nadhani zinapaswa kuheshimu utawala wa Sheria uliopo Tanzania lakini wanaweza kutusema pale tu wanapoona hatufuati sheria zetu, lakini kwa hili (la kukamatwa Wakili Boniface Mwabukusi, Mdude Nyagali na Dk. Slaa) taratibu zote za kisheria zimefuatwa,” alisema Prof. Mkumbo na kuongeza kuwa:

“Jumuiya za kimataifa zinapaswa kutupa nafasi ya kufuata katiba na sheria zetu. Lakini pia nafahamu hakuna nchi dunaini inayovumilia au kulea uhalifu,” amesema.

Amesema wao kama Serikali wanaheshimu mawazo na hisia za Watanzania katika suala la uwekezaji wa bandari lakini kwa uzoefu wake hakuna mwekezaji yeyote mkubwa na mzuri ambaye alifika Tanzania kuwekeza na hakupingwa au kukutana na upinzani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles