26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mkumbo atoa ushauri kuhusu mabadiliko Sheria ya Habari

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WADAU wa habari nchini, wametakiwa kujipanga pale watakapoitwa na kamati husika ya bunge kutetea mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya habari, wawe na hoja nzito.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Ubungo, Profesa. Kitila Mkumbo, alipozungumza na Waandishi wa Habari bungeni jijini Dodoma kuhusu mchakato wa mabadiliko ya sheria hiyo iliyotungwa mwaka 2016.

Prof. Mkumbo amesema kwa kawaida wadau wa habari watakutana na kamati na kule ndio wanapaswa kueleza hoja zao kwanini wanadhani baadhi ya vifungu hivyo vinapaswa kubadilishwa.

“Wadau wa habari wanatakiwa kujipanga ili watakapokuja kwenye kamati husika waweze kutoa hoja zao kwanini wanataka baadhi ya vifungu katika Sheria ya Huduma za Habari 2016 viboreshwe.

“Unafahamu kwenye kamati ndio wadau wanapata nafasi ya kutoa hoja zao kwanini wanataka baadhi ya vipengele vifanyiwe marekebisho,” amesema Prof. Mkumbo.

Akizungumzia mchakato huo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema ingawa mpaka sasa hajajua wakati ambao mapendekezo hayo yatafikishwa bungeni, lakini bado ana matumaini kwamba safari ya mabadiliko hayo haitaishia njiani.

Mwenyekiti wa Jukuwaa la Wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile.

Balile amesema, Serikali bado inaonesha kuwa na dhamira njema ya kufanya mabadiliko.

“Waziri wa Habari ndiye mwenye kujua lini watapeleka bungeni muswada lakini sisi wadau tumepewa fursa ya kutoa maoni yetu.

“Tumeona dhamira njema ya serikali hadi hivi sasa, tukiendelea hivi nadhani huko tuendako tutashirikiana vizuri kwa masilahi ya Taifa letu,” amesema Balile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles