25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI YANASA MMOJA UTEKAJI WATOTO

Na JANETH MUSHI-ARUSHA

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limemkamata mtuhumiwa mmoja anayedaiwa kuhusika na utekaji wa watoto jijini hapa, aliyekimbilia mkoani Geita.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo, alisema kuwa waliendesha operesheni kali kuwakamata watuhumiwa wanaohusika na vitendo hivyo vilivyojitokeza siku za hivi karibuni na kuzua hofu kwa wazazi.

Watoto hao ni Maurine David(6),ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi, Lucky Vincent,aliyetekwa tangu Agosti 21 mwaka huu na Ikram Salim(3),aliyetekwa Agosti 25 mwaka huu.

“Kuna mmoja alikimbilia Geita tulimfuata kule na amekamatwa usiku, alienda huko akateka mtoto mwingine huko kwa bahati nzuri sisi tulikuwa tuna m-track tukamkamata.Wewe subiri kwa sababu tunaendesha operesheni kali ili tuwakamate wote, kesho mchana (leo), tutakuwa na nafasi ya kuzungumza juu ya matukio hayo,”alisema Kamanda Mkumbo

Watoto wanne walitekwa na wawili kati yao hawajapatikana mpaka sasa ambao ni Maurine David (6),ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi, Lucky Vincent,aliyetekwa tangu Agosti 21 mwaka huu na Ikram Salim (3),aliyetekwa Agosti 25 mwaka huu.

Watoto wengine ambao walitekwa ni Ayub Fred (3) na Bakari Selemani (3) wote wawili wazazi wao wanaishi Mtaa wa FFU Kata ya Muriet jijini hapa,ambao walipatikana Agosti 28 mwaka huu.

Watoto hao walipatikana baada ya watekaji hao kuwasiliana na wazazi wao kupitia balozi wa eneo lao ambapo waliwarudisha kwa njia ya pikipiki.

 

WANANCHI OLASITI WAFANYA MSAKO

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Olasiti ambako  walikuwa wakiishi watoto Maurine na Ikram,wameanza msako wa kuwatafuta watoto hao juzi na kufanikiwa kukamata watu wawili.

Akizungumza na MTANZANIA, Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, kata ya Olasiti, Daudi Safari alisema kuwa wananchi pamoja na wazazi wa watoto hao, David Njau na Salim Kassim,wameamua kuwasaka watuhumiwa hao.

Alisema kuwa walifanikiwa kumkamata wakala wa Mpesa ambapo watuhumiwa hao walitoa Sh. 300,000 zilizokuwa zimetumwa na Babu wa Ikram pamoja na kinyozi (majina yanahifadhiwa),ambaye simu yake ilitumiwa na watekaji hao kuomba fedha.

“Tulijaribu pamoja na wazazi kutafuta wakala ambapo pesa hiyo ilitolewa huku eneo la  Kwa Morombo ila kuna namba wale wahalifu walitumia kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kuwa itumwe m- pesa,pamoja na kinyozi wa  saluni ambaye simu yake ilitumika kutuma ujumbe ambaye alikiri mtu huyo kuwahi kunyoa kwake zaidi ya mara nne,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles