26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi wapambana na wananchi Njombe

Na Francis Godwin, Njombe

JESHI la Polisi jana lililazimika kutumia zaidi ya saa 5.00 kupambana na wananchi waliokuwa wakiandamana bila kibali wakitaka kuchukua maiti ya mmoja wa wakazi wa Njombe aliyedaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi hilo wakati wa msako wa wanywa pombe.

Mtu huyo inaelezwa alifariki dunia juzi na mwili wake kuhifadhiwa katika Hospitali ya Kibena.
Inaelezwa wananchi hao walikuwa wakiandamana kuuchukua mwili wa marehemu huyo na kuupeleka polisi.

Wakizungumzaia tukio hilo, baadhi ya wananchi walisema juzi saa 3.00 usiku polisi walivamia kilabu cha pombe kilichopo Zenge Mtaa wa Kambarage na kuwakamata watu zaidi ya 20 waliokuwa wakilewa kilabuni hapo.

Baada ya wananchi hao kukamatwa wakiwamo wahudumu, inadaiwa polisi hao waliokuwa wamevalia ‘kininja’ waliwapiga raia walioonyesha kukaidi agizo la kutaka kutoa fedha walizokuwa nazo kama faini ya kunywa pombe usiku huo.

Kijana mmoja, Bashiri Mwalongo, ambaye alikuwa akitaka akitaka kutoka mlangoni alijikuta akipigwa na kitu kinachosadikika kuwa risasi tumboni na kufa papo hapo.

Inaelezwa kuwa Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), jana walilazimika kuwatawanya waandamanaji hao kwa mabomu ya machozi.
Wananchi hao walikuwa wanataka kwenda kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi, kuwasilisha malalamiko yao.

Vurugu hizo zilisambaa na kusababisha baadhi ya shughuli za jamii yakiwamo maduka mjini Njombe kufungwa.

Mashuhuda walisema vurugu hizo zilisababisha barabata Kuu ya Njombe – Ruvuma na Iringa ya Njombe – Iringa na Njombe – Makete kufungwa na waandamanaji hao ambao walichoma matairi ya magari katikati ya barabara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, alishindwa kuzungumza na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi wa vurugu hizo kwa vile alichukua muda mrefu kwa kuwa katika kikao na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles