25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Polisi wafanya mazoezi kuimarisha afya, ulinzi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala limefanya mazoezi kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuimarisha afya pamoja na ulinzi na usalama.

Mazoezi hayo ya viungo yalianzia Buguruni na kuhitimishwa Tabata huku yakihusisha pia vijana wa jogging.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala, Afisa Mnadhimu Mkoa wa Kipolisi Ilala, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Moses Fundi, amesema mazoezi yana faida kubwa kwani yanapunguza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyoambukiza kama vile presha kisukari, saratani na kuongeza uwezo wa kufikiri.

“Ukifanya mazoezi hata akili yako inafanya kazi vizuri, mazoezi yanapunguza uwezekano wa kuzeeka ni rai yangu kwa wananchi wawe na utamaduni wa kufanya mazoezi angalau nusu saa kila siku badala ya kusubiri kuja kuambiwa na wataalam kwamba wafanye mazoezi,” amesema Fundi.

Naye Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Buguruni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Thedius Kaihuzi, amesema mazoezi yanadumisha mahusiano mema baina ya jeshi hilo na wananchi.

“Tunafanya mazoezi ili tuimarishe miili yetu iwe ‘fit’ kwa sababu ili tuweze kupambana na uhalifu askari anatakiwa awe ‘fit’ kiafya pamoja na kiakili. Vilevile kunapokuwa na vikundi vya ulinzi shirikishi na vijana wa jogging ni sehemu ya kuhimizana masuala ya ulinzi shirikishi ili kuhakikisha maeneo yetu yanakuwa salama,” amesema Kaihuzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata, Colle Senkondo, amesema jukumu la kupambana na wahalifu hawalifanyi peke yao bali wanashirikiana na wananchi ndiyo maana katika mazoezi hayo walishirikina pia na vikundi vya ulinzi shirikishi na jogging.

“Katika kutekeleza majukumu yetu tunatakiwa tuwe na afya njema ili tuweze kukabili mapambano ya uhalifu na tuna ushirikishwaji wa jamii kwa sababu wahalifu wako kwenye mitaa na maeneo mbalimbali hivyo inakuwa rahisi kupata taarifa,” amesema Colle.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles