25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

POLISI UGANDA WAMSHIKILIA MTUHUMIWA KIFO CHA RADIO

KAMPALA, UGANDA



JESHI la Polisi Uganda linamshikilia anayedaiwa kumpiga na kumsababishia kifo msaanii, Mowzey Radio.
Mtuhumiwa Godfrey Wamala, alikamatwa eneo la Kyengera Wilaya ya Wakiso juzi baada ya msako uliokuwa ukifanywa na kikosi maalumu cha polisi kilichokuwa kikiongozwa na Kamanda Frantile Lwamusaayi.

Kifo cha mwanamuziki huyo kilitokana na kipigo kikali kilichothibitishwa na Hospitali ya Case wiki iliyopita jijini Entebbe.

Radio kabla ya kifo chake alipigwa na kuzimia akiwa katika ukumbi wa starehe wa De Bar, uliopo jijini Entebbe Januari 22, mwaka huu.

Baada ya kukamatwa Wamala jana jioni alitarajiwa kufikishwa kituo cha polisi cha Katwe ambapo atatoa maelezo kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Entebbe.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles