24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI MWANZA WAZUIA DISCO TOTO

Na BENJAMIN MASESE-MWANZA

JESHI la Polisi mkoani Mwanza limezuia  kumbi zote za starehe kuwapo na disco toto na kutoa tahadhari kwa atakeyepuuza agizo hilo atachukuliwa hatua kali zakisheria.

Pia limewataka viongozi wa Serikali za mitaa kuacha mara moja kutoa barua za kuwadhamini watu wanaokamatwa kwa uhalifu hususan  vibaka na watu wanaotumia silaha, ili waweze kukaa ndani na kuchukuliwa hatua za kisheria wakiwa chini ya vyombo vya dola.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ahmed Msangi, alisema hatua hiyo imechukuliwa ikiwa  ni sehemu ya kuzuia  madhara yanayoweza kujitokeza kwa watoto hasa katika sikukuu za Krismas na mwaka mpya.

Alisema jeshi la polisi limejipanga kuimarisha ulinzi katika jiji hilo ambapo litaanza kufanya doria kuanzia usiku wa kuamkia leo na atakayekutwa akifanya uhalifu ama kuwa na ni ovu, atachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

“Naomba niwatahadharishe wale ambao wana mawazo ya kufanya fujo, ubakaji, uhalifu wa aina mbalimbali kama kupora ama kuwasha matairi na kuharibu miundombinu ya barabara na majengo, hao tutakula nao sahani moja, naomba kila mmoja asheherekee krismas na mwaka mpya kwa amani.

“Tumejipanga vilivyo kila kona, pia tumesambaza askari wetu mitaa kadhaa kwa ajili ya kuangalia mienendo ya jamii maeneo hayo, hivyo wananchi watambue kila walifanyalo macho yetu yanaona, kikumbwa naomba kuzuia kuwapo na kumbi za disco za watoto katika kumbi za starehe, atakayekiuka atakiona cha mtema kuni,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles