29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Pluijm atoa onyo Yanga

plijmNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Hans Van Der Pluijm, amewaonya viongozi wa klabu hiyo na kuwataka wahakikishe wanafanya usajili utakaoiletea timu mafanikio na siyo ubabaishaji.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alisema kipindi cha usajili kimekuwa na matukio ya ajabu ambayo hupelekea mipango ya mwalimu kuvurugika kutokana na viongozi kufanya maamuzi yao binafsi.
Pluijm ambaye anatarajia kuondoka nchini Jumamosi kuelekea Ghana kwa ajili ya mapumziko na mikakati ya msimu ujao wa ligi na michuano ya Klabu Bingwa, alisema wanahitaji maandalizi mazuri zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita.
“Maandalizi ya msimu ujao yanatakiwa kuwa makubwa zaidi ya ilivyokuwa kipindi hiki tulichomaliza, haitawezekana kama viongozi watashindwa kufanya usajili wa kuleta maendeleo na siyo maonyesho,” alisema Pluijm.
Pluijm alisema tayari ameshakabidhi ripoti yake kwa uongozi na mahitaji, hivyo jukumu limebaki kwao kuijenga au kuibomoa timu hiyo.
“Nimeshafanya majukumu yangu na kukabidhi ripoti, kazi kwao sasa kuijenga timu kwa kufanya usajili wa uhakika au kubomoa kwa kusajili wachezaji wasio na mwelekeo,” alisema Pluijm.
Mholanzi huyo aliendelea kusema upande wake anaamini kikosi alichokipendekeza msimu ujao kitafanya mambo makubwa zaidi.
Alisema ubingwa wa klabu hiyo ni changamoto tosha kwa viongozi kuonyesha umakini wa kuendeleza timu itakayotetea taji na kuleta mataji mengi ya michuano ya kimataifa.
Kocha huyo anayetarajia kuondoka Jumamosi, atarejea nchini Juni 7 mwaka huu kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles