25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm apanga mauaji Zanzibar

yngNA SAADA AKIDA, ZANZIBAR

KOCHA Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans Van Der Pluijm, amepanga kuifanyia mauaji timu ya JKU katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Mapinduzi utakaofanyika leo visiwani Zanzibar, huku akidai hatadharau timu yoyote iliyofikia hatua hiyo.

Wakati Yanga ikiwa na shughuli pevu kuvaana na JKU, Azam nayo itachuana vikali na Mtibwa Sugar, huku mabingwa watetezi KCCA wakicheza na Polisi Zanzibar kwenye Uwanja wa Amaan.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alieleza kushtushwa na matokeo ya ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Shaba waliocheza nao juzi, hali iliyompa changamoto ya kutodharau timu yoyote iliyoingia hatua ya robo fainali.

Alisema Shaba walionyesha kiwango cha hali ya juu ingawa walishindwa kufikia malengo yao kwa kupoteza mchezo huo, huku akidai mchezo huo umempa picha halisi ya kujipanga vyema na kuwa makini hatua ya robo fainali.

Katika hatua ya makundi, Yanga ilifanikiwa kuzifunga timu zote ilizokutana nazo, ambapo ilianza kwa kuilaza timu ya Taifa Jang’ombe mabao 4-0, baadaye ikaichapa Polisi Zanzibar idadi kama hiyo ya mabao kabla ya kuichapa Shaba kwenye mchezo wa mwisho.

“Ukiangalia katika mechi mbili za hatua ya makundi tulipata ushindi mnono wa mabao 4-0 katika kila mchezo, lakini tulipokutana na Shaba tulipoteza nafasi nyingi za wazi na kuibuka na ushindi wa bao 1-0,” alisema.

Yanga ambayo haijaruhusu bao katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, itachuana vikali na JKU ambayo inapewa nafasi ya kufanya vizuri kwa upande wa Zanzibar kutokana na umahiri wa kikosi chake tangu kuanza kwa michuano hiyo.

Yanga imepania kuendeleza ubabe katika Kombe la Mapinduzi ili kujiimarisha zaidi na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) na ile ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles