33.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda: Ndugu msichukue mali za marehemu

Mizengo-Pinda1Na WALTER MGULUCHUMA, KATAVI

WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, amewataka Watanzania kuachana na mila zinazoruhusu ndugu kuchukua mali za marehemu.

Badala yake, ametaka mila hizo zizuie utaratibu huo ili mali hizo zitumiwe na mke na watoto wa marehemu.

Pinda aliyasema hayo juzi wakati wa mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kasansa Halmashauri ya Mpimbwe, Wilaya ya Mlele,  Sixto Chalahani.

“Ndugu wa marehemu wanapaswa kuachana na utamaduni huo wa kugombania mali za  marehemu kwani unasababisha mjane wa marehemu na watoto kuhangaika .

“Watoto na mjane aliyeachwa na marehemu, wanaendelea na masomo na kama mali zilizochwa na marehemu zitakwisha, jamii iendelee kusaidia kadiri inavyowezekana.

“Katika Kabila la Wapimbwe ninalotoka mimi, mwanamume anapofariki, tuna utamaduni wa ndugu wa upande wa mume kugawana mali za marehemu na kuwaacha   mjane na watoto wa marehemu wakihangaika mitaani.

“Kwa hiyo, naomba tuache utaratibu huu kwa sababu si mzuri na unarudisha nyuma maendeleo,” alisema Pinda.

Wakati huo huo, Pinda aliwataka wananchi wa kata hiyo kuanza kujiandaa na uchaguzi  mdogo kwa kufikiria ni nani atakuwa diwani  wao atakayeendeleza aliyoacha marehemu Chalahani.

Chalahani alikuwa ni Diwani wa Kata ya Kasansa tangu mwaka 2010 hadi alipofariki Agosti 23 mwaka huu, akitibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles