24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda kuwa mgeni rasmi ufunguzi wa Nanenane Kanda ya Mashariki

Na Gustafu Haule, Pwani

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda,anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya siku ya wakulima (Nanenane )Kanda ya Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti Mosi, mkoani Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa  wanaounda Kanda ya Mashariki ametoa taarifa hiyo leo Ijumaa Julai 28, wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika ofisi yake iliyopo Mjini Kibaha.

Kunenge amesema maonesho ya Kanda ya Mashariki yanajumuisha mikoa mikubwa minne ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro na kwamba tangu kuanzishwa mwaka 1993  mwaka huu ni maonesho ya 30.

Amesema kuwa maandalizi ya maonesho hayo yamekamilika na kwamba mwaka huu yatakuwa maonesho ya mfano kutokana na kila mkoa unaoshiriki maonesho hayo kujipanga vizuri pamoja na wadau kuongezeka kwa asilimia 20.

Aidha, Kunenge ameongeza kuwa kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Vijana na Wanawake na Msingi Imara na Endelevu kwa Chakula” ambayo inaendana na jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya uzalishaji na kulisha dunia.

Kunenge amesema lengo la maonesho hayo ni kuakisi malengo ya wananchi ili wafikie pale wanapotakiwa na kuongeza tija katika uzalishaji k katika sekta ya kilimo,uvuvi na ufugaji.

“Kanda ya Mashariki mwaka huu tumejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanapata mbinu mpya za uzalishaji katika kilimo,uvuvi na ufugaji na yeyote anayekuja hakika atakuwa ameongeza kwa kujifunza mambo mengi na hivyo kuongeza tija  katika shughuli,” amesema Kunenge.

Amesema kila mkoa umekuwa na mkakati kabambe wa kutambulisha mazao mapya ya kimkakati ambapo miongoni mwa mazao hayo ni muwa, mkonge, mchikichi ambapo tayari wameweka mkakati katika kuwainua wakulima kupitia mazao hayo.

Kunenge amesema mbali na kuwepo kwa maonesho  ya masuala ya kilimo,uvuvi na ufugaji lakini kutakuwa na wanyama mbalimbali kama simba, ngamia, chui, twiga ambapo wananchi wanaweza kufanya utalii maalum.

“Sisi tumeyafanya maonesho yetu kuwa sehemu ya kujifunza mambo mengi, ukiachia masuala ya kilimo lakini pia kutakuwa na utalii mzuri wa wanyama adimu kama simba na wengineo lakini burudani pia zitakuwepo,” amesema Kunenge.

Pia amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika kutembelea maonesho hayo kwakuwa yapo mambo mengi ya msingi yanayolenga kuboresha kilimo, ufugaji na uvuvi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles