31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda azitaka benki kwenda vijijini

Waziri-Mkuu-wa-Tanzania-Mizengo-Pinda1Na Michael Sarungi, Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema sasa umefika wakati wa benki kuwa rafiki wa wananchi vijijini.

Amesema kwa sasa nchi za Afrika zinahitaji kuwaleta wananchi wa maeneo ya vijijini kuanza kuwa rafiki wa benki kama njia ya kuwainua katika uchumi.

Alitoa kauli hiyo alipofungua mkutano wa wataalamu wa sekta ya benki wa nchi za Afrika, Dar es Salaam jana. Hotuba yake ilisomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Christopher Chiza.

Alisema madhumuni ya mkutano huo ni kuziwezesha nchi wanachama kuweza kukaa pamoja kujadili masuala mbalimbali muhimu yanayoikabili sekta hiyo.
“Tunahitaji kuwaleta wananchi hasa wa maeneo ya vijijini kuanza kuwa marafiki wa benki ili mwisho wa siku wajikwamue katika uchumi.

“Muungano huu wa benki za akiba duniani ulianzishwa mwaka 1925 lengo ikiwa ni kuziwezesha nchi wanachama kuweza kubadilishana uzoefu katika tasnia ya benki,” alisema.

Alisema mkutano huo unatarajia kutoa azimio la pamoja la jinsi ya kukabiliana na changamoto hasa katika nchi nyingi za Afrika ambazo bado hazijawa na miundombinu bora.

Alisema wananchi wengi katika bara la Afrika bado kwa kiwango kikubwa hawajawa na mwamko wa kuweka akiba ndani ya benki.

“Tunahitaji mkutano huu uje na njia mbadala ya kuweza kuwafikia wananchi wa kawaida hasa katika maeneo ya vijijini ili mwisho wa siku waweze kukopesheka.

Mkurugenzi wa Benki za Akiba Duniani, Chris de Noose, alisema Afrika bado inakabiliwa na changamoto ya miundombinu linapokuja suala la uwekezaji jambo linalohitaji ufumbuzi wa haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles