22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda atamani sheria ya wosia

Mizengo-PindaJonas Mushi na Adam Mkwepu, Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema kuna haja ya kuwa na sheria itakayowezesha uandikishaji wosia kuwa wa lazima ili kuondokana na migogoro ya kugombania mali za marehemu na unyanyasaji wa wajane na watoto.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana, katika maadhimisho ya miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) na uzinduzi wa kampeni ya uandishi wa wosia.
Alisema migogoro hiyo kwa kiasi kikubwa inaathiri wanawake na watoto pindi wazazi wa kiume wanapofariki.
“Kama inawezekana nawaomba TAWLA muanzishe mchakato wa kutengeneza sheria ya wosia ili iwe lazima kwa kila mtu kuandika wosia na mimi nitawapa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha suala hilo linafanikiwa,” alisema Pinda.
Alisema kuna dhana potofu kuwa kuandika wosia ni kujitabiria kifo, huku wengine wakihofia kuwa wakiandika wosia watauliwa na wanufaika wa wosia ili wamiliki mali walizoachiwa.
“Wananchi watambue kuandika wosia kunasaidia kuondoa matatizo pale mzazi mmoja anapofariki na si uchuro kama wengi wanavyodhani ni kujitabiria kifo,” alisema Pinda.
Alisema wosia huwa ni siri ya anayeandika na hautakiwi kuwekwa wazi kwa wanufaika, isipokuwa kwa mwanasheria na mashahidi wawili ambao huweka bayana mgawanyo wa mali pindi mwandika wosia anapofariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles