21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Picha| Bodi ya ATF na Kamishina ya TACAIDS zakutana kujadili masuala muhimu katika mwitikio wa UKIMWI

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko akifafanua lengo la TACAIDS kukutanisha Bodi hizo mbili za ATF na ile ya Kamisheni ambazo zote zinaisimamia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma Mei 25, 2022
Wajumbe wa Kamisheni, wajumbe wa Bodi ya ATF na Menejimenti walioshiriki kikao cha pamoja kwa lengo la kufahamiana pamoja na kujadili majukumu ya Bodi zote mbili, majukmu ya TACAIDS, muundo na tathimini ya utekelezaji wa Mkakati wa nne (MNSF IV), vipaumbele vya mkakati wa tano wa Kudhibiti UKIMWI Tanzania(NMSF V) na matokeo yanayotegemewa pamoja na mpango wa utekelezaji wa ATF na Mapendekezo ya kuboresha vyanzo vya fedha vya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Richard Ngirwa akiwasilisha tathimini ya utekelezaji wa Mkakati wa nne (MNSF IV), vipaumbele vya Mkakati wa tano wa Kudhibiti UKIMWI Tanzania(NMSF V) na matokeo yanayotegemewa katika kikao cha Kamisheni na bodi ya ATF kilichofanyika tarehe 25Mei,2022 jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamisheni ya TACAIDS, Dk. Sajida Kimambo akizungumzia umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa huduma za kutokomeza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kutoka kushoto ni Prof. Magreth Bushesha na kulia kwake ni Bahati Haule. Wote ni makamishina wa TACAIDS.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI(ATF), Caroline Mdundo akijadili ajenda ya muundo wa TACAIDS baada ya kuwasilishwa na wataalam, wakati wa majadiliano katika kikao hicho kilichokutanisha bodi ya ATF na Kamisheni Mei 25, 2022 jijini Dodoma.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles