25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Phiri awapa tahadhari viongozi Simba

Kikosi cha Simba
Kikosi cha Simba

NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Mzambia Patrick Phiri, ameutahadharisha mapema uongozi wa klabu hiyo kutomuingilia katika mipango yake ya kujenga kikosi bora.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, Phiri alisema kikosi chake kimeweka kambi Zanzibar kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara. Alisema viongozi wanapaswa kumuacha atekeleze majukumu yake mwenyewe na si kuingiliwa.

Alisema anatambua kama viongozi wanachokihitaji ni ushindi, lakini ni vizuri wakafahamu kuwa mafanikio hayaji kwa maneno tu.

“Sitapenda kuona naingiliwa hata kidogo katika majukumu yangu, nasema hivi kwa kuwa naifahamu Simba tangu kipindi kile nilipokuwepo,” alisema Phiri.

Alisema atahakikisha wachezaji wote aliowakuta wanaelewa na kufanya vizuri katika ligi.

Phiri ameingia mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha Simba baada ya kutimuliwa kwa Zdravko Logarusic.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles