27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Phiri awafungia kazi kina Sserunkuma

Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri
Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri

 

 

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM,
KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Patrick Phiri amewafungia kazi wachezaji wake wapya hasa wale wa kigeni ili kuangalia kwa umakini viwango vyao, ikiwa ni sehemu ya mikakati yake kuona anaweza kuwatumia vipi na kwa mfumo gani katika kikosi chake.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Phiri alisema baada ya usajili wa dirisha dogo angependa kufahamu kwa kina uwezo wa kila mchezaji mpya ili mwisho wa siku aweze kujua jinsi ya kuwatumia.
Alisema kuwa japo alishawaona walipocheza na Yanga mwishoni mwa wiki iliyopita katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, lakini mechi moja haitoshi kutoa picha halisi ya uwezo wa mchezaji kwa ujumla wake.
“Ninahitaji kuwafahamu zaidi kuona uwezo wao ili nijue ni vipi ninaweza kuwatumia katika kikosi changu, lakini pia ni mfumo gani utafaa kulingana na aina ya uchezaji wao,” alisema Phiri.
Mzambia huyo alisema mwishoni mwa wiki hii, atapata fursa nyingine ya kuwasoma zaidi wachezaji hao wakati watakapoivaa timu ya Ligi Daraja la Kwanza ya Mwadui, inayonolewa na kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’.
Katika mchezo huo utakaopigwa Jumamosi katika uwanja ambao hadi sasa haujajulikana, Phiri ameahidi kuwatumia wachezaji wote wapya.
Baada ya mchezo huo, kikosi kizima cha Simba kitakwenda Zanzibar kuweka kambi kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, zaidi ukiwa ni mchezo wao wa raundi ya nane dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Desemba 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles