25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Peru waifuata Brazil fainali Copa America

PORTO ALEGRE, BRAZIL

TIMU ya taifa ya Peru imefanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Copa America baada ya kuwachapa mabingwa watetezi Chile mabao 3-0.

Peru walipewa nafasi ndogo kuweza kutinga hatua hiyo ya fainali baada ya kupangiwa Chile kwenye mchezo wa nusu fainali, lakini wameishangaza dunia baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu na kufanikiwa kuingia fainali.

Chile walipewa nafasi kubwa kutokana na uzoefu wa michuano hiyo huku wakiwa mabingwa watetezi baada ya kutwaa taji hilo mara mbili mfululizo, lakini jana hawakuwa na ujanja mbele ya wapinzani hao.

Chile walitaka kuandika historia mpya ya kutwaa taji hilo mara tatu mfululizo kama ambavyo ilifanywa na Argentina mwaka 1940, lakini wameshindwa na sasa wanakwenda kuwania nafasi ya tatu dhidi ya Argentina Jumamosi. Argentina iliondolewa kwenye hatua ya nusu fainali dhidi ya wenyeji Brazil kwa kichapo cha mabao 2-0.

Hii ni mara ya kwanza kwa Peru kufanikiwa kuingia hatua hiyo ya fainali baada ya kufanya hivyo mwaka 1975, ambapo ni miaka 44 sasa.

Hata hivyo, Peru wamefika hapo baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi kwa ‘Best Loser’ lakini baada ya hapo wamekuwa wakileta ushindani wa hali ya juu.

Wameingia hatua ya fainali baada ya kuwaondoa Uruguay kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya dakika 90 kumalizika kwa timu hizo bila kufungana.

Kutokana na matokeo hayo ya jana, Peru wanakwenda kukutana na wenyeji wa michuano hiyo Brazil katika mchezo wa fainali ambao utapigwa Jumapili wiki hii kwenye uwanja wa Maracana.

Huo utakuwa mchezo wa kisasi baada ya Brazil kuwachapa wapinzani hao mabao 5-0 kwenye mchezo wa hatua ya makundi, hivyo Peru wanajipanga kwa ajili ya kulipiza kisasi, wakati huo Brazil wakiamini wanaweza kufanya kama walivyofanya kwenye mchezo huo wa hatua ya makundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles