23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Pembejeo zakwamisha wakulima wa korosho

20Na Florence Sanawa, Mtwara
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, imetoa siku 10 kwa mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao la korosho kuhakikisha kuwa pembejeo zinawafikia wakulima ili waweze kuwahi kupulizia dawa hizo msimu huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe, alisema usambazaji wa pembejeo hizo umemtia mashaka kutokana na wilaya tatu za Masasi, Mtwara Halmashauri na Tandahimba kukosa pembejeo hizo kwa wakati unaotakiwa.
Alisema Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara, imefuatilia na haijaridhishwa na kasi ya ugawaji wa pembejeo unaofanywa na mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao la korosho na mawakala bila kuzingatia muda wa ugawaji huo.
Akwilombe alisema kuwa baada ya Halmashauri Kuu kuangalia athari zinazoweza kujitokeza za ucheleweshaji wa usambazaji wa pembejeo baada ya mfuko huo kubeba jukumu la kusambaza badala ya mfumo wa awali wa vyama kutafuta mawakala wa kusafirisha pembejeo hizo.
Hata hivyo, Akwilombe aliongeza kuwa zaidi ya asimilia 65 ya pembejeo za korosho hutumika Mkoa wa Mtwara hivyo Halmashauri Kuu ya chama hicho imetoa ushauri pembejeo hizo kuletwa kwa kutumia Bandari ya Mtwara, badala ya kufikia Bandari ya Dar es Salaam kisha kuletwa Mtwara kwa barabara.
Aliongeza kuwa CCM inawakumbusha viongozi na watumishi wote wanaohusika na taasisi, idara au asasi zinazoshughulikia zao hilo kuwajibika na kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mapema na kwa haraka.
Akwilombe alisema zao la korosho ndio maisha ya wana Mtwara hivyo wawe macho na makini na maisha yao kwa kuangalia na kushughulikia korosho kwa uzito stahiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles