26.4 C
Dar es Salaam
Friday, December 20, 2024

Contact us: [email protected]

Paula amwangukia Kajala

MTOTO wa mwigizaji, Kajala Masanja anayeitwa Paula, amemwandikia ujumbe mama yake kupitia WhatsApp Status, akimwomba radhi kwa kutofanya vizuri katika mitihani yake licha ya mwigizaji huyo kujitoa na kumwonyesha upendo mkubwa.

 “Mpendwa mama najua sikustahili, najua ulikuwa mtu mwema niliyewahi kumfahamu katika maisha yangu, kwa ufupi wewe ni ‘role model’ wangu, najua siku zote sikuwa mtoto bora na nina uhakika nilifanya iwe ngumu zaidi kuliko ilivyotakiwa,

“Nilikuwa nawaonea wivu rafiki zangu ambao walikuwa na wazazi wao wote pamoja sababu ni kitu ambacho sikuwahi kukipata lakini nikagundua nina kitu ambacho wao hawana, asante kwa kutonikatia tamaa, asante kwa maelfu ya shilingi ulizotumia kwenye elimu yangu, najua tumepitia kipindi kigumu lakini hujawahi kuacha kunipenda,” aliandika Paula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles