32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

PARIS JACKSON: NATAMANI KUACHA KUVUTA SIGARA LAKINI NASHINDWA

Na BADI MCHOMOLO

UKIWA unakumbwa na msongo wa mawazo mara kwa mara unaweza kufanya mambo ambayo utakuja kuyajutia katika maisha yao kama utashindwa kuwa makini na kufanya maamuzi sahihi juu ya mawazo ambayo yanakusumbua.

Wadau wengi wa muziki duniani waliguswa na kifo cha staa wa muziki wa Pop nchini Marekani, Michael Jackson, ambacho kilitokea Juni 25, 2009. Wapo ambao walipoteza fahamu baada ya kupata taarifa ya kifo cha msanii huyo.

Msanii huyo aliacha watoto watatu ambao ni Michael Joseph Jackson Jr mwenye umri wa miaka 20, Paris Jackson mwenye umri wa miaka 18 na Prince Michael Jackson II mwenye miaka 15. Kila mmoja kati ya wote hao waliguswa sana na kifo hicho cha baba yao, lakini ilikuwa tofauti kwa Paris ambaye alionekana kama anataka kuchanganyikiwa.

Kipindi Jackson anapoteza maisha Paris alikuwa na umri wa miaka 11, alikimbizwa hospitalini baada ya kupata taarifa ya kifo hicho cha baba yake, lakini baada ya muda alirudi katika hali ya kawaida, ila kila mara alikuwa anaonekana akiwa na mawazo, hivyo alikuwa anasimamiwa na wataalamu wa kuondoa mawazo ili aweze kuwa sawa.

Tangu hapo alianza kufikiria kuvuta Sigara huku akiwa na lengo la kutaka kupunguza mawazo ya baba yake na kuna wakati alikuwa anafikiria kunywa pombe ili alewe sana na apate usingizi akiwa na lengo la kupoteza ndoto za mara kwa mara juu ya baba yake.

Alishindwa kunywa pombe kwa kipindi hicho, lakini aliweza kuvuta sigara kwa kujificha sana, uvutaji wa kujificha mara kwa mara ulimfanya aizoee sigara, lakini baada ya kufikisha miaka 17 alianza kuonekana wazi kuwa anavuta sigara.

Majimbo mbalimbali nchini Marekani yamekuwa yakipiga marufuku uvutaji wa sigara kwa vijana wenye umri chini ya miaka 18, hata hapa Tanzania, lakini kwa Paris akiwa na miaka hiyo 17 alikuwa anavuta mitaani na kukumbana na misukosuko ya kila mara na polisi.

Alikuwa na furaha sana baada ya Aprili mwaka jana kutimiza miaka 18, hivyo aliamua hatoweza kujificha tena katika uvutaji wa sigara, ni wazi alikuwa anavuta kila kona jambo lililomfanya kuathirika na uvutaji wa sigara.

Familia yake ilijaribu kukaa naye pamoja na kumshauri kuachana na uvutaji wa sigara lakini aliwajibu kuwa anatamani kuachana na uvutaji lakini anashindwa kabisa na alianza kuvuta kutokana na kutaka kupunguza mawazo ya baba yake, lakini kwa sasa anashindwa kuacha.

“Mawazo yanaweza kukuweka katika mazingira magumu ndani ya maisha yako, wakati nina umri wa kuanzia miaka 11 nilikuwa katika wakati mgumu baada ya kumpoteza baba yangu kipenzi, nilifikiria kufanya mambo mengi ambayo ni mabaya katika maisha yangu kama vile kunywa pombe, kuvuta sigara na mambo mengine.

“Lakini kikubwa ambacho nilikifikiria na nikakifanya ni kuvuta sigara, jambo ambalo lilikuwa baya zaidi kwa kuwa nilikuwa na umri mdogo, hivyo limeniharibu na hadi sasa najaribu kutaka kuacha lakini ninashindwa.

“Nikikaa muda mrefu bila kuvuta sigara najisikia vibaya, lakini ninaamini kama ningeweza kuzuia hisia zangu katika kipindi cha kifo cha baba yangu basi nisingekuwa kwenye hali nilionayo kwa sasa na sipendi kuwaona vijana wadogo wakifikiria kuvuta sigara,” alisema Paris.

Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya, mbali na Paris kujitaja kuwa anashindwa kuachana na uvutaji wapo wengi ambao wameathirika na uvutaji wa sigara na wanashindwa kuacha, hilo ni tatizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles