Mshindi wa kwanza katika bahati nasibu ya Parimatch, Fred Chacha, kutoka Geita (katikati) akivaa kofia ngumu ya pikipiki wakati wa kukabidhiwa pikipiki yake aliyoshinda kupitia michezo ya bahati nasibu kwa njia ya tovuti na maduka ya kampuni hiyo yaliyofanyika katika ofisi zao leo Jumatatu Julai 29, jijini Dar es Salaam.
Parimatch yawazawadia washindi 10 wa mchezo wa bahati nasibu
Kampuni ya Parimatch inayojihusisha na michezo ya bahati nasibu kwa njia ya tovuti na maduka imepata washindi 10 kutoka mikoa mbalimbali nchini na kukabidhi zawadi hizo kwa washindi hao.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni hiyo, Tumaini Maligana amesema kampuni hiyo ambayo ni mpya na ya kisasa zaidi inaendesha michezo hiyo ya bahati nasibu kwa gharama ndogo zaidi ya kuanzia Sh 300 pekee.
Amesema wana maduka 12 ambayo yanatumia mbinu za kisasa katika uendeshaji wa michezo hiyo na wateja wanaweza kubeti hata mechi moja kwa gharama nafuu.
“Kampuni yetu tunaiendesha kisasa zaidi na hiyo ni kutokana na ukuaji wa teknolojia, tunapatikana kwa njia ya mtandao ya www.parimatch.co.tz na tunatumia kompyuta katika kuendesha michezo hiyo ya bahati nasibu na si karatasi kama ilivyozoeleka,” amesema Maligana.
Aidha, amesema michezo ya kubahatisha kwao ni burudani na si ajira kama inavyotafsiriwa na baadhi ya watu wanaoendesha michezo hiyo kwa ustaarabu wa hali ya juu.
Washindi hao waliopatikana kupitia mbio za Afcon wamejishindia zawadi mbalimbali ambapo mshindi wa kwanza amejishindia pikipiki, mshindi wa pili na watatu wamejishindia Smart TV na mshindi wa nne hadi 10 wamejishindia simu za kisasa za mkononi (smart phone.)
Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo Fred Chacha, kutoka Geita ambaye amejishindia pikipiki ameeleza kufurahishwa na namna mchezo huo ulivyoendeshwa hadi akaibuka mshindi na kujishindia pikipiki ambayo itampa ajira na amewashauri vijana wengine kutumia michezo hiyo kama burudani na sio ajira kama ilivyozoeleka.