23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

PAPA FRANCIS, UN WAMKOSOA TRUMP KUHUSU YERUSALEM

NEW YORK, MAREKANI



KIONGOZI wa Kanisa la Katoliki Duniani Papa Francis na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres wamekosoa hatua ya Rais Trump kuutambua mji wa Yerusalem kuwa makao makuu ya Israel.
Akizungumza na Shirika la Habari Marekani (CNN), Guterres alisema hatua hiyo inaleta wasiwasi katika mpango wa kutafuta suluhu ya mgogoro baina ya Palestina na Israel.
Guteeers ametoa msimamo huo siku ambayo pia msemaji wa Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence aliishutumu Serikali ya Palestina.
Msemaji huyo alisema hakufurahiswa na kitendo cha Rais wa Palestina Mahmoud Abbas kugoma kukutana na Pence kufuatia mzozo wa mji wa Yerusalem.
Waandamanaji wameendelea kukusanyika mitaani katika nchi za Kiaarabu wakipinga hatua hiyo ya raia Trump.
Naye Papa Francis ambaye anaongoza Wakatoriki bilioni moja duniani ametoa maoni yake, akisema Yerusalem ni mji mtakatifu kwa Wakristo, Wayahudi na Waislami.

Kwa sababu hiyo, anasema uamuzi wa Trump haukuwa sahihi na kwamba ni mazungumzo pekee yanayoweza kuleta suluhu katika mzozo huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles