32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Onyesho la Nane la SITE kuanza Oktoba 11

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) katika kutangaza Vivutio vya Utalii na fursa mbalimbali za Uwekezaji zilizopo nchini imeandaa Onesho la nane la Site kwa mwaka 2024 litakalofanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Septemba 12, 2024 jijini Dar es na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Ephraim Mafuru alisema Onesho hilo litahudhuriwa na waoneshaji wa bidhaa na huduma za Utalii zaidi ya 120 sambamba na wanunuzi wa bidhaa na huduma za Utalii takribuni 120 kutoka Nchi ambazo ni kimkakati ya utalii wetu ikiwemo nchi za Asia, Ulaya na Amerika.

Alisema onesho hilo litshusisha utangazaji wa bidhaa mbalimbali za utalii, jukwaa la uwekezaji, semina kuhusu masuala ya utalii na masoko na mikutano ya wafanyabiashara za utalii.

“Onesho la Site linakwenda sambamba na utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 pamoja na mkakati wa kutangaza utalii kimataifa 2020 -2025 ambayo imetilia mkazo kuitangaza Tanzania kam kivutio bora cha utalii duniani,” alisema.

Alieleza kuwa Onesho hilo linafuatiwa na ziara za mafunzo “FAM trips” ambayo yanalenga kuwajengea uelewa wanunuzi wa hidhaa na huduma za utalii kuhusu vivutio vyetu vya utalii ili waweze kuvitangaza katika nchi zao na dunia kwa ujumla.

Alitoa rai kwa wadau wa utaliii waliopo ndani na nje ya nchi hususani Wakala wa biashara za utalii,watoa huduma za malazi, Wakala wa safari na zingenezo kushiriki na kuchangamkia fursa za kiuchumi na kijamii zitokanazo na Onesho la Site 2024.

Onesho la Site litakalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Expole Tanzania for a life Time Investment and Seamless Tourism Experience”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles