25.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisa TRA kortini akidaiwa kumiliki mali ya mil. 700/-

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

OFISA Forodha Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA), Godfrey Mapunga, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya kumiliki mali isiyoendana na kipato chake yenye thamani ya Sh milioni 721.

Mshtakiwa alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  jana na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi , Vitalius Peter akisaidia na Lilian William mbele ya Hakimu Mwandamizi, Salum Ally,.

Lilian alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya April Mosi, 2011 na Julai 19, 2016 eneo la Ubungo akiwa mtumishi wa umma.

Anadaiwa kumiliki nyumba ya ghorofa moja eneo la Goba Manispaa ya Ubungo, yenye thamani ya Sh 698,921,217, ambayo haiendani na kipato chake cha sasa na cha zamani.

Wakili William alidai katika kipindi hicho, mshtakiwa anadaiwa kumiliki kiwanja kimoja ambacho hakijasajiliwa kilichopo eneo la Mbezi Juu katika Manispaa ya Ubungo, chenye thamani ya Sh milioni saba.

Vilevile, anadaiwa kumiliki ardhi ambayo haijasajiliwa iliyopo eneo la Kigamboni, yenye thamani ya Sh milioni sita.

Mshtakiwa pia anadaiwa kumiliki kiwanja ambacho hakijasajiliwa kilichopo   Goba , chenye thamani ya Sh milioni 9.5.

Jumla anadaiwa kumiliki  ambazo haziendani na kipato chake cha sasa na cha zamani, za Sh 721,421,217.

Mshtakiwa alikana shtaka na Hakimu Ally alitaja masharti ya dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo kuwaanatakiwa awasilishe fedha taslimu Sh 360,710,608 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Pia mshtakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya ahadi kila mmoja ya Sh 360,710,608.

Sharti jingine ni kuwa mshtakiwa hauruhusiwi kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama  na kuwasilisha hati yake ya kusafiria.

Mshtakiwa alishindwa kutumiza masharti ta dhamana na hivyo kurudishwa rumande.  Mshtakiwa atasomewa maelezo ya awali Januari 29, 2019.

Wakati huohuo, watumishi wanne wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamepandishwa kizimbani katika mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizire, wakidaiwa kusababisha hasara ya Sh 58,390,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles