30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisa elimu mbaroni tuhuma za rushwa

Mwandishi Wetu-Singida

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), inawashikilia Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani hapa, Albert Ngimba na mwenzake mmoja kwa makosa ya kushawishi na kutoa hongo ya Sh 500,000 kwa ofisa uchunguzi wa taasisi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda alisema azma hasa ya watuhumiwa kutenda kosa hilo ilikuwa  kumshawishi ofisa  wa taasisi hiyo awasaidie kwenye uchunguzi unaohusiana na tuhuma za ufujaji na ubadhirifu wa fedha zilizotolewa na Serikali Kuu.

Alimtaja mtuhumiwa mwingine wa sakata hil, kuwa ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Isenengwa wilayani humo, George Mmembwa ambao kwa pamoja walishiriki  ufujaii wa fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya nyumba za walimu na vyoo .

“Watuhumiwa hawa walikamatwa juzi saa 8 usiku nyumbani kwa ofisa  wa Takukuru wakiwa wamepelekea kiasi hicho cha pesa kama sehemu ya shilingi milioni 4 waliyokuwa wamemuahidi,” alisema.

Alisema uchunguzi wa tuhuma hizo, bado unaendelea na  utakapokamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2007.

“Takukuru mkoa wa Singida inatoa wito kwa wananchi kuongeza kasi ya ushirikiano kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa, pia kujitokeza mahakamani pindi wanapohitajika kutoa ushahidi wao,” alisema Elinipenda.

Katika hatua nyingine katika kipindi cha Januari na Aprili, mwaka huu, ofisi ya taasisi hiyo imewapandisha kizimbani watuhumiwa wapatao 13 wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali za vitendo vya rushwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles