23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Patel amwaga vifaa vya Sh mil 6

Gustaphu Haule ,Pwani

MFANYABIASHARA maarufu na mmiliki wa makampuni ya M.M.I Steel Limited nchini Subhash Patel, ametoa msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 6.

Msaada huo, ulikabidhiwa juzi na msaidizi wa mfanyabiashara  huyo, Aboubakary Mlawa kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo mjini Kibaha.

Mlawa alikabidhi seti 25 za matanki ya kunawia maji ambapo kila seti moja ikigharimu Sh 250,000 na vitatumika  maeneo mbalimbali ya mkoani hapa.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Mlawa alisema  msaada huo ni sehemu ya mchango wa Patel  kusaidiana na Serikali kupambana na maambuzi ya virusi vya ugonjwa wa COVID-19 ili kuweza kuzuia vifo vya wananchi.

Alisema  Kampuni ya M.M.I, inatoa msaada huo mikoa mbalimbali na maeneo mengine nchini, lakini Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mpango huo kwakuwa inarudisha sehemu ya faida kwa wananchi.

“Mapambano dhidi ya kujikinga na COVID-19 ni jukumu letu sote ndio maana Subhash Patel ameamua kushirikiana na Serikali katika mapambano hayo kwa kutoa vifaa vya kunawia maji yakiwemo matanki ya lita 200 hivyo naomba mpokee,”alisema Mlawa.

Naye  Mhandisi Ndikilo,alimshukuru mfanyabiashara huyo kwa msaada aliotoa kwakuwa unalengo la kuleta usalama kwa wananchi dhidi ya kujikinga na maambukizi ya COVID-19.

Alisema atasimamia vifaa hivyo ili vifanyekazi iliyokusudiwa na kwamba vifaa hivyo vitapelekwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa ili kusaidia Wananchi kupata unafuu wa kujikinga na ugonjwa huo.

Alitaja baadhi ya maeneo yatakayopelekwa vifaa, kuwa ni Hospitali ya Rufaa Tumbi,Hospitali ya Wilaya Bagamoyo,Soko la Loliondo Kibaha Mjini,Kituo cha afya Kibiti, Hospitali ya Wilaya ya Rufiji-Utete,kituo cha afya Mkoani, Mlandizi,Mkuranga,na kituo cha matibabu cha COVID -19 kilichopo Lulanzi Kibaha mjini.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles