Na Upendo Mosha,Rombo
Makundi makubwa ya Nyani, Ngedere na Tumbili kutoka katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro na hifadhi jirani ya nchini Kenya yamevamia mashamba na makazi ya watu wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro na kuharibu mazao na kula wanyama wafugwao.
Akiwasilisha kero hiyo Mbunge wa Jimbo la Rombo, Prof. Adolf Mkenda wakati wa ziara ya kikazi ya waziri wa Maliasili na Utalii, Damian Ndumbaru, amesema katika maeneo ya vijiji mbalimbali yamevamiwa na wanyama pori hao na kuketa uharibifu mkubwa Katika mazao.
Amesema wanyama hao pamoja na kuharibu mazao ya wakulima pia wamekuwa wakishambilia na kula wanyama wafugwao kama mbuzi, kondoo na kujeruhi watoto hali ambayo imekuwa ikihatarisa usalama wao hususani wanafunzi.
“Wanyama hawa wamekuwa wakileta madhara kwa wananchi hasa wakulima wamevamia mashamba na wengine wanakula Mbuzi jambo hili Ni hatari lazima itafutwe njia ya kuwafukuza kwa usalama bila kuwadhuru,”amesema.
Akizungumzia suala hilo diwani wa kata ya Kitangara Mrere, Venance Maleli, amesema wanyama hao wamegeuka kero na kuiomba serikali kuwasaidia waanchi kuwafukuza kwaniwameharibu mazao ya chakula.
“Wanyama hawa wamekuwa wakifuatana kwa makundi Kati ya mia moja hadi mia mbili na wananchi wamekuwa wakiwafukuza bila mafanikio na wanaharibu mazao mashambani…tunawafukuza wanakimbilia kwenye miti mirefu na kurejea tena,”alisema maleli
Anaeli Kimaro ambaye ni mkazi wa Kijiji Cha Mrere amesema pamoja na wanayama hao kuharibu mashamba wamekuwa wakiiba watoto na kukimbia nao Katika miti Jambo ambalo limezidi kuhatarisha usalama wa watoto.
“Wanyama wanachukua hadi watoto wetu…mmoja alichukuliwa hadi juu ya mti tulimuoko kwa shidah linatutishia sana jambo hilo serikali itusaidie kwa kuwa tunapata shida,” amesema.
Akijibu kilio cha wananchi hao, Dk. Ndumaro amesema wanyama hao hawawezi kuuliwa kutokana na kutegemewa Katika shughuli za utalii na kwamba serikali itafanya mpango wa kuwaondoa.
“Naagiza mamlaka ya wanyamapori(TAWA) kuwafukuza wanyama hawa na kuwarudisha katika hifadhi na mbuga za wanayama ili kuondoa kero na usumbugu kwa wananchi na kufanya msako wa mara kwa mara,”amesema.